Lugha Nyingine
Sanaa za Mikono za kale zaoneshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Sanxingdui mkoani Sichuan, China (7)
Kichwa cha shaba kikioneshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Sanxingdui huko Guanghan, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China Julai 21, 2024. (Xinhua/Tang Wenhao) |
Maonesho yaliyopewa jina la “Ufundi wa Sanaa za Mikono na Ustadi: Kuonesha Mafanikio ya Uhifadhi na Urejeshaji tena wa Mabaki ya kale ya Kiutamaduni yaliyofukuliwa hivi karibuni kutoka Eneo la Kihistoria la Sanxingdui” yamefunguliwa mkoani Sichuan, China siku ya Jumanne.
Zaidi ya kazi 50 zilizorejeshwa upya katika hali ya awali za vyombo vya shaba, vyombo vya dhahabu, vyombo vya jade, vyombo vya meno ya ndovu na mabaki mengine ya kale zinaoneshwa katika maonesho hayo, ambayo yataendelea hadi mwisho wa mwaka 2024.
Yakiwa yaligunduliwa mwishoni mwa miaka ya 1920 kwenye Mji wa Guanghan, Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, Magofu ya ustaarabu wa Sanxingdui, yametajwa kuwa moja kati ya ugunduzi mkubwa zaidi wa kiakiolojia duniani katika karne ya 20.
Taasisi ya Utafiti wa Mabaki ya Kale ya Kiutamaduni na Akiolojia ya Mkoa wa Sichuan siku ya Jumanne ilisema kuwa, kuanzia mwaka 2022, maeneo ya kihistoria zaidi ya 400 yamebainishwa, ikiwemo misingi ya kiwango cha juu ya majengo, mashimo ya majivu, mitaro ya majivu na maeneo ya kihistoria ya uzalishaji na usindikaji sanaa za mikono za mawe katika eneo hilo la Sanxingdui. Sanaa za kazi za mikono zaidi ya 4,000, vikiwemo vyombo vya udongo, vya jade na vya mawe zimefukuliwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma