Lugha Nyingine
Wakazi wa Mji wa Chongqing, China wajipoza joto ndani ya hifadhi ya wakati wa mashambulizi ya anga (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 18, 2024
Siku ya Jumatano, Julai 17 Mji wa Chongqing, China ulitoa tahadhari ya hali joto kali ya ngazi ya rangi ya machungwa, ambayo ni tahadhari ya ngazi pili kwa hali joto kali zaidi na wakazi wengi walikwenda kwenye hifadhi ya wakati wa mashambulizi ya anga ili kujipoza miili na kupata huduma za mapumziko.
Imeripotiwa kuwa, ili kukidhi mahitaji ya wakazi ya kujipoza miili wakati wa joto, vituo 39 vya kujipoza miili vya hifadhi ya raia wakati wa mashambulizi ya anga katika maeneo 11 ya mji huo wa Chongqing vimefunguliwa kwa umma bila ya malipo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma