Lugha Nyingine
Mashindano ya wapanda farasi ya Michezo ya 12 ya Makabila Madogo ya China yaanza
URUMQI – Mashindano ya wapanda farasi katika Michezo ya 12 ya Kitaifa ya Jadi ya Makabila Madogo ya China yameanza siku ya Jumatatu huko Zhaosu, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, China ambapo mashindano hayo ya wapanda farasi, ambayo ni ya mapema zaidi kuanza katika michezo hiyo ya mwaka huu, yataendelea hadi Julai 13 na kushirikisha idadi kubwa zaidi ya timu, zikiwa na wanamichezo 229 kutoka ujumbe wa makabila 12.
Mashindano hayo yanajumuisha shughuli za mashindano na maonyesho. Shughuli za mashindano zinajumuisha mbio za jadi za farasi, urushaji mishale wa wapanda farasi, unyakuzi wa hada na mbio za farasi za mtu mmoja mmoja. Na zile za maonyesho zimegawanywa katika mashindano ya kiufundi na yale jumuishi.
Katika mbio za farasi za jadi za mita 2,000, Tashi Phuntsok kutoka Mkoa unaojiendesha wa Xizang alivuka mstari wa kumaliza kwanza.
"Naona fahari kushindana hapa na kushirikiana na wapanda farasi kutoka mikoa na makabila mbalimbali," amesema.
"Nimejiandaa kwa mashindano haya kwa miaka minne, na nimefurahia kuwa nimefanya kwa uwezo wangu wote."
Michezo hiyo ya makabila madogo ya China itafanyika kuanzia Novemba 22 hadi 30 huko Sanya, Hainan.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma