Lugha Nyingine
Kundi la Watafiti washuhudia idadi kubwa ya nyangumi na pomboo kwenye eneo la bahari la Mashariki la Kisiwa cha Hainan, China (4)
Pomboo aina ya Fraser wakiogelea katika eneo la bahari la Mashariki ya Kisiwa cha Hainan, China tarehe 6, Julai. |
Hivi karibuni, kundi la watafiti wa “wanaofuatilia nyangumi ‘Haitang’ na Bionuwai ya Baharini" wameshuhudia idadi kubwa ya nyangumi na pomboo kwenye eneo la bahari la Mashariki la Kisiwa cha Hainan, China, wakiwemo nyangumi wa jamii ya kujiongoza katika makundi wenye mapezi mafupi na pomboo aina ya Fraser.
Watafiti hao wameeleza kuwa, kundi la nyangumi na pomboo hao waliowashuhudia mara hii linajumuisha jozi nyingi za mama na mtoto, hali ambayo inaonesha bioanuwai tajiri ya Bahari ya Kusini mwa China.
Shughuli hiyo ya utafiti imefanywa kwa pamoja na Idara ya Bahari ya Hainan, Idara ya Mambo ya Kilimo na Vijiji ya Sanya, Taasisi ya Sayansi na Uhandisi wa Bahari ya Kina ya Akademia ya Sayansi ya China, na Jumuiya ya Ulinzi wa Bahari ya Utepe wa Bluu.
(Picha na Zhang Liyun/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma