Lugha Nyingine
Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Beijing yafunguliwa na washiriki kutoka nje ya China waongezeka (2)
Mhariri wa vitabu Wei Guangqi (Kati) akitambulisha kitabu kuhusu Vichochoro vya Hutong vya Beijing kwenye Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Vitabu ya Beijing, Juni 19, 2024. (Xinhua/Luo Xiaoguang) |
BEIJING - Maonyesho ya 30 ya Kimataifa ya Vitabu ya Beijing yamefunguliwa siku ya Jumatano mjini Beijing, China yakivutia waonyeshaji wengi wa kigeni kushiriki kwenye maonesho hayo ikilinganishwa na mwaka jana, ambapo eneo la maonyesho hayo limepanuliwa kwa mita za mraba 55,000 mwaka huu, maonyesho hayo ya siku tano yamekusanya waonyeshaji wapatao 1,600 kutoka nchi na maeneo 71, yakionyesha machapisho 220,000 ya Kichina na ya lugha za kigeni kwa watembeleaji wake, waandaaji wa maonyesho hayo wamesema.
Maonesho hayo yameshuhudia ongezeko la washiriki 150 wa ng’ambo ikilinganishwa na mwaka uliopita, washiriki kutoka nje ya nchi wamefikia 1050, wakichukua asilimia 66 ya washiriki wote.
Ikilinganishwa na Mwaka 2023, maonyesho hayo ya mwaka huu yamekaribisha nchi mpya 15 zinazoshiriki, zikiwemo Azerbaijan, Qatar, Jamhuri ya Czech, Slovakia na Nigeria.
Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Beijing yaliyoanzishwa mwaka 1986, ni moja ya maonyesho makubwa zaidi ya vitabu duniani na yanatumika kama jukwaa kuu la mawasiliano kati ya mashirika ya uchapishaji, kuwezesha biashara ya machapisho kutoka China na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuchapisha vitabu na kazi za media.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma