Lugha Nyingine
Kampuni za Saudi Arabia na China zafanya majaribio ya teksi za kuruka angani (2)
Watu wakipanda teksi ya kuruka angani inayojiendesha bila dereva wakati wa majaribio yaliyofanyika huko Mecca, Saudi Arabia, Juni 12, 2024. (Kampuni ya Front End/Xinhua) |
RIYADH - Kampuni za Saudi Arabia na China zimefanikiwa kufanya majaribio ya kujiendesha kwa teksi ya kwanza ya kuruka angani bila dereva huko Mecca, Saudi Arabia ambapo majaribio hayo yamefanywa siku ya Jumatano na Kampuni ya Front End, kampuni ya Saudi Arabia iliyobobea katika kuunganisha teknolojia ya hali ya juu katika sekta mbalimbali, kwa ushirikiano na EHang, kampuni ya jukwaa la teknolojia ya vyombo vya kiotomatiki vya kuruka angani ya China.
Majaribio hayo yanalenga kuongeza kasi, ufanisi, na uendelevu wa usafiri wakati wa ibada ya Hija, ambayo ni ibada takatifu ya kila mwaka ya waumini wa dini ya Kiislamu kwenda Mecca, mji mtakatifu zaidi kwa Waislamu.
Abdulaziz Al-Duailej, Mwenyekiti wa Mamlaka Kuu ya Usafiri wa Anga ya Saudi Arabia, amesema, "Majaribio hayo yameonesha maendeleo makubwa katika utekelezaji wa mpango wa Usafiri wa Hali ya Juu wa Angani katika mazingira ya anga ya Saudi Arabia."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma