Lugha Nyingine
Meli ya kwanza ya kiwango cha tani 10,000 iliyofikia eneo la mtiririko wa juu la Mto Changjiang yawasili Bandari ya Jiangjin Luohuang, China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2024
CHONGQING - Meli ya kiwango cha tani 10,000 ya usafiri wa bahari ya mbali imewasili katika Mji wa Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China siku ya Jumatano, na kuwa meli ya kwanza yenye ukubwa wa namna hiyo kusafiri hadi eneo la mtiririko wa juu wa Mto Changjiang.
Meli hiyo ya “Uvumbuzi No.5” iliyobeba chakula chenye uzito wa tani zaidi ya 5,000, iliondoka kutoka Bandari ya Zhoushan ya Ningbo katika mkoa wa pwani wa mashariki wa Zhejiang Aprili 24. Imesafiri kupitia njia ya moja kwa moja ya mtoni-baharini ya Chongqing-Zhoushan, ambayo inaunganisha moja kwa moja mji huo wa Chongqing katika eneo la mtiririko wa juu wa Mto Changjiang na bahari.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma