Lugha Nyingine
Eneo la kihistoria lililostawishwa?la Mto Yuehe lawa kivutio cha watalii katika Mji wa Jiaxing, Mashariki mwa China (5)
Watalii wakipumzika na kuonja chai kwenye eneo la kihistoria la Mto Yuehe, Wilaya ya Nanhu, Jiaxing, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, tarehe 26 Aprili 2024. (Xinhua/Xu Yu) |
Eneo la kihistoria la Mto Yuehe lililo katika Wilaya ya Nanhu, Jiaxing, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, ambalo lina sehemu yenye ukubwa wa mita za mraba 90,000, historia yake inaweza kuanzia katika Enzi za Ming na Qing (1368-1911) za China ya kale. Huku Mfereji Mkuu wa Beijing-Hangzhou, mito ya Waiyue na Liyue ikipita kwake, eneo hilo ni eneo kamili na kubwa zaidi la kihistoria katika Mji wa Jiaxing ambalo linaweza kuonyesha vyema umaalumu wa makazi na wa utamaduni wa mji wa maji huko "Jiangnan," eneo lenye mandhari nzuri kusini mwa Mto Yangtze.
Tangu Mwaka 2003, hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa ili kurejesha ustawi wa eneo hilo: majengo ya jadi ya makazi yenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya 80,000 yamerejeshwa kwa mtindo wa jadi, na sekta ya utalii imeendelezwa ikichukua faida za urithi wa kihistoria za eneo hilo.
Siku hizi, eneo hilo la kihistoria la Mto Yuehe linapokea watalii wapatao milioni 5 kila mwaka na kuwa kivutio maarufu cha utalii katika eneo hilo. (Xinhua/Xu Yu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma