Lugha Nyingine
Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa ya China yafunguliwa na idadi ya wanunuzi wa ng'ambo yaongezeka sana (3)
GUANGZHOU - Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa ya China, ambayo pia yanajulikana kwa jina la Maonyesho ya Canton, yamefunguliwa Jumatatu huko Guangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, ambapo hadi kufikia Jumapili, wanunuzi takriban 149,000 kutoka nchi na maeneo 215 walikuwa wamejiandikisha mapema kwa ajili ya kutembelea maonyesho hayo, ikionesha kidhahiri idadi ya wanunuzi wa ng'ambo imeongezeka kwa asilimia 17.4 ikilinganishwa na maonyesho yaliyotangulia.
Shauku ya wanunuzi wa ng'ambo kushiriki imeongezeka, huku kukiwa na kuongezeka kwa wanunuzi kutoka Marekani, nchi za Mashariki ya Kati, nchi zinazoshiriki Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na nchi wanachama wa Ushirikiano wa Pande Zote wa Kiuchumi wa Kikanda (RCEP).
Yakiwa yamepangwa kufanyika hadi Mei 5, maonyesho hayo yana mabanda takriban 74,000 ya maonyesho, huku waonyeshaji zaidi ya 29,000 wakitarajiwa kushiriki.
Eneo la maonesho hayo ni lenye ukubwa wa mita za mraba milioni 1.55, maonyesho hayo yanahusisha bidhaa za sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na viwanda vinavyotumia teknolojia za kisasa, magari yanayotumia nishati mpya, betri za lithiamu, na seli za nishati ya jua.
Waandaaji wamepanga shughuli zaidi ya 600 za kutangaza biashara, wakipanua zaidi wigo na ufikiaji wa maonyesho hayo.
Maonesho hayo yalianzishwa Mwaka 1957, ambayo yanafanyika mara mbili kwa mwaka, na yanachukuliwa kuwa kipimo kikuu cha biashara ya nje ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma