Lugha Nyingine
China iko tayari kurusha satelaiti ya kupokezana ya Queqiao-2 (4)
WENCHANG, Hainan – Mkusanyiko wa vyombo vya satelaiti ya kubadilishana ya Queqiao-2 na roketi ya kubeba mizigo kwenda anga ya juu ya Long March-8 Y3 kwa pamoja vimehamishwa kiwima siku ya Jumapili hadi eneo la kurusha roketi kwenye Kituo cha Urushaji Vyombo kwenda Anga ya Juu cha Wenchang katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China.
Shirika la Anga ya Juu la China (CNSA) limesema kuwa, Satelaiti hiyo inatarajiwa kurushwa kwa wakati ufaao ndani ya siku chache zijazo.
Mkusanyiko wa vyombo hivyo umehamishwa nje ya jengo la majaribio la wima asubuhi, na kisha kuwasilishwa kwa usalama hadi eneo lao la kurushwa.
Ukaguzi wa roketi, kazi ya majaribio ya pamoja na ujazaji wa kani utafanywa kabla ya urushaji, shirika la CNSA limesema.
Queqiao-2, au Daraja la Magpie -2, itatumika kama jukwaa la kupokezana kwa kipindi cha nne cha mpango wa utafiti wa China wa sayari ya Mwezi kwa kutoa huduma za mawasiliano kwa vyombo vya Chang'e-4, Chang'e-6, Chang'e-7, na Ujumbe wa Chang'e-8.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma