Lugha Nyingine
Kituo cha usambazaji kilichojengwa na China chazinduliwa nchini Ethiopia kuhimza biashara ya mtandaoni (5)
Picha iliyopigwa Februari 29, 2024 ikionesha mashine ya kuainisha bidhaa katika Kituo cha usambazaji cha biashara ya mtandaoni huko Addis Ababa, Ethiopia tarehe 29, Februari, 2024. (Picha/Xinhua) |
Shirika la ndege la Ethiopia limezindua kituo kipya cha usambazaji wa biashara ya mtandaoni mjini Addis Ababa, ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wanunuzi na wauzaji reja reja mtandaoni.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana Alhamisi waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Ethiopia Alemu Sime, amesema kituo hicho kinalenga kurahisisha utendaji na usimamizi kabla ya bidhaa kutumwa kwa wateja. Kituo hicho kilichojengwa na kampuni ya China, kina eneo la takriban mita za mraba 15,000 na kina uwezo wa kushughulikia tani laki 1.5 za bidhaa kwa mwaka.
Ofisa Mkuu mtendaji wa Shirika la Ndege la Ethiopia Bw. Mesfin Tasew amesema kuzinduliwa kwa kituo hicho baada ya ujenzi wa miaka miwili, kunathibitisha kujitolea kwa shirika hilo la ndege kuendana na ubunifu na teknolojia zinazoibukia, na kuimarisha utoaji wa huduma zake.
Daraja la kuvuka Mto Yangtze la Longtan likiendelea kujengwa huko Nanjing, China
Watawa 12 wapata shahada yenye hadhi sawa na uzamivu katika Ubuddha wa Tibet, China
Sherehe kwenye hekalu zafanyika Mkoa wa Henan katikati ya China
Boti nyingi zafanya safari baharini katika Mji wa Sanya, Mkoani Hainan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma