Lugha Nyingine
Sanaa ya maigizo ya karagosi yenye historia ya miaka 2,000 yakaribisha mwaka mpya huko Shandong, China (3)
Mwaka mpya kwa kalenda ya kilimo ya China umekaribia. Jiang Yutao, ambaye ni mrithi wa kizazi cha tano wa sanaa ya “Maigizo ya Karagosi ya Laixi” katika Wilaya ya Laixi, Mkoa wa Shandong, China ameongoza kundi lake la wasanii kuandaa na kupanga maigizo, ili kuonesha kwa umma maigizo mapya ya karagosi kwa wakazi wa huko wakati wa mwaka mpya.
Sanaa ya karagosi ya Wilaya ya Laixi ina historia ya zaidi ya miaka 2,000. Kwa kuendana na sifa za nyakati na mahitaji ya umma, Jiang ameboresha mchakato wa utengenezaji wa karagosi, akabuni maigizo mapya na kuingiza mambo mengine kama vile hekaya, katuni na hadithi za kichimbakazi, ili kuufanya uwasilishaji wa maigizo ya karagosi kuwa na maana zaidi katika maisha ya hivi sasa, na kupendwa na vijana. (Picha na Zhang Jingang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma