Lugha Nyingine
Xi Jinping na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam wakutana na wawakilishi wa vijana wa China na Vietnam na watu waliochangia urafiki wa nchi hizo (2)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mkewe Peng Liyuan pamoja na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam Nguyen Phu Trong na mkewe walikutana na wawakilishi wa vijana wa China na Vietnam na watu wanaochangia urafiki wa nchi hizo mbili Mchana wa tarehe 13, Desemba kwa saa za Vietnam.
Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu yenye kichwa cha “Kuendeleza urafiki wa jadi na Kuanza safari mpya ya Kujenga Jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja”, ambapo amesisitiza kuwa, msingi wa urafiki wa nchi hizo mbili ni watu wao, na mustakabali wa nchi hizo mbili unategemea vijana.
Ametoa matumaini matatu kwa vijana wa China na Vietnam: Kwanza, wanaweza wote kuwa warithi wa urafiki wa nchi hizo mbili na kuchangia nguvu zao katika kujenga jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja wa umuhimu wa kimkakati. Pili, kufanya juhudi ili kuwa washiriki katika ustawishaji wa eneo la Asia-Pasifiki, na kuchangia usalama na utulivu endelevu wa eneo hilo. Tatu, ni kuthubutu kuwa vinara wa kuongoza maendeleo ya binadamu, na kufanya juhudi bila kuchoka kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Kwa upande wake, Nguyen Phu Trong amesema, mustakabali wa uhusiano wa China na Vietnam unategemea vijana. Kwamba, anatumai vijana wa nchi hizo mbili wataelewa kwa kina, kurithi na kuendeleza urafiki wa jadi ulioanzishwa na viongozi wa kizazi cha zamani, na kuingiza nguvu mpya katika kuhamasisha maendeleo ya muda mrefu yenye utulivu ya uhusiano wa kiwenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa Vietnam na China, na ukuaji endelevu wa mambo ya ujenzi ya kijamaa ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma