Lugha Nyingine
Pilikapilika ya ujenzi wa paneli za kuzalisha?umeme kwa jua katika Jangwa la Tengger huko Zhongwei, Ningxia, China (3)
Kwa mujibu ripoti za habari, Mradi wa Kituo cha Nishati Mpya cha Jangwa la Tengger wa Mkoa wa Ningxia nchini China ni kituo cha nishati mpya chenye uwezo wa kuzalisha umeme wenye uwezo wa kilowati makumi ya mamilioni jangwani na Kituo cha Nishati Mpya cha Gobi kilichopangwa na kujengwa na serikali ya China. Pia ni kituo cha kwanza cha China cha kupitisha umeme wenye nguvu ya juu zaidi kinachojikita katika kuzalisha umeme kwa jua katika jangwa kubwa na kusafirisha nishati mpya. Awamu ya pili ya mradi huo ulioanza wakati huu uko kwenye ukingo wa kusini mashariki mwa Jangwa la Tengger, na ukubwa wa eneo lake ni takriban hekta 4000.
Baada ya mradi huo kukamilika na kuunganishwa kwenye gridi ya taifa ya China, utaweza kuzalisha umeme wenye uwezo wa kilowati bilioni 3.96 kwa saa kila mwaka, kuokoa makaa ya mawe ya kawaida yenye uzito wa tani milioni 1.207, na kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni kwa uzito wa tani takriban milioni 3.2938. Ni muhimu sana katika kuwezesha ujenzi wa mfumo wa nishati iliyo safi, yenye kutoa kaboni chache, salama na fanisi. (Picha na Yuan Hongyan /Tovuti ya Picha ya Umma)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma