Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China atoa wito wa kuboreshwa kwa maeneo ya majaribio ya biashara huria (FTZs) na uchunguzi wa ufunguaji mlango wa kiwango cha juu
SHANGHAI - Waziri Mkuu wa China Li Qiang ametoa wito wa kutekeleza kwa nguvu mkakati wa kuboresha maeneo ya majaribio ya biashara huria (FTZs), na kufanya uchunguzi mpya wa ufunguaji mlango wa kiwango cha juu.
Waziri Mkuu Li, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa wito huo alipofanya ziara ya ukaguzi mjini Shanghai Jumatano na Alhamisi.
Kwenye ziara yake katika eneo la biashara huria la Eneo Maalum la Lin-gang la Shanghai, Waziri Mkuu Li amehimiza ufunguaji mlango kwa kina na katika nyanja pana zaidi, na kutoa wito wa kuwepo kwa maendeleo zaidi katika ujenzi wa majukwaa yenye ufanisi, na mazingira ya viwanda na biashara.
Amesisitiza umuhimu wa usimamizi wa data za kuvuka mipaka, na kuahidi kuvutia kampuni zaidi za kigeni kuwekeza nchini China, na kutaka juhudi za pamoja za kuhakikisha minyororo ya viwanda na ugavi iimarike, na kuhimiza maendeleo ya kundi la viwanda.
Akihudhuria kongamano, Waziri Mkuu Li alisikiliza ripoti kutoka kwa maafisa wakuu wa Wizara ya Biashara ya China na wa maeneo manane ya ngazi ya mkoa na amesisitiza sana umuhimu wa maeneo ya majaribio ya biashara huria katika mageuzi na ufunguaji mlango wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma