Lugha Nyingine
Jeshi la Anga la China lafanya Maonesho ya Urukaji wa Ndege kuwakaribisha makadeti wapya (7)
Shughuli ya wazi ya Maonyesho ya urukaji wa ndege ya Jeshi la Anga la China 2023 ya Changchun imeanza kufanyika huko Changchun, China Julai 26. Vikosi mbalimbali vimefanya pamoja maonesho ya angani ya urukaji wa ndege na kuruka kwa parachuti. Jeshi la Anga la China liliwakaribisha makadeti wapya kwenye “Uwanja wa Anga ya Bluu” kwa heshima ya kipekee, na kuvutia vijana wengi zaidi kutoa mchango wa nguvu zao za ujana kwa ajili ya kulinga anga buluu ya taifa.
Kwenye ufunguzi, ndege za kivita za J-20, J-16, Y-20 na nyingine mbalimbali zilionekana moja baada ya nyingine. Shughuli hiyo imeonesha mafanikio ya Jeshi la Anga la China katika kuharakisha ujenzi wa jeshi la anga la kiwango cha juu duniani.
Picha zimepigwa na Tan Sicheng na kuchapishwa na Shirika la Habari la China, Xinhua.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma