Lugha Nyingine
Zaidi ya wasanii 1,000 waleta sanaa ya kale kwenye tamasha la dansi la Xinjiang (5)
URUMQI - Tamasha la 6 la Kimataifa la Dansi la China Xinjiang limefunguliwa Alhamisi huko Urumqi, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, na kuvutia wasanii kuonyesha dansi zao kwenye uwanja wa kimataifa.
Tamasha hilo lenye kaulimbiu isemayo "Ndoto za Dansi, Maelewano ya Njia ya Hariri," limevutia wasanii zaidi ya 1,000 kutoka Asia, Ulaya na Afrika. Tamasha hilo litafanyika kwa siku 17 na kuhusisha maonyesho 60.
Maonyesho hayo yanajumuisha aina za sanaa kama vile ballet, maonesho ya dansi ya kijadi, na maonesho ya michezo ya Sanaa ya muziki. Miongoni mwao kutakuwa na maonesho maarufu ya dansi ya ballet ya China "Kikosi cha Wapiganaji Wanawake " na maonesho ya dansi ya ballet "The Sleeping Beauty" inayowashirikisha wacheza dansi wa Belarus.
Shughuli mfululizo zitafanyika wakati wa tamasha hilo, ikiwa ni pamoja na maonyesho ya dansi za mraba.
Likiwa lilianzishwa Mwaka 2008, tamasha lake la 6 linaandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China, Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, na serikali ya Mkoa wa Xinjiang.?
Sarakasi za kijadi zang'ara katika Mji wa Wuqiao, mkoani Hubei, Kaskazini mwa China
Mji wa Qingzhen wa China: Mandhari Nzuri ya Milima na Maziwa Yaonekana wazi
Katika Picha: Sao Tome na Principe yaadhimisha miaka 48 tangu kupata uhuru wake
Picha: Mandhari Nzuri ya eneo la msitu wa mawe wa Zecha huko Luqu, Kaskazini Magharibi mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma