Lugha Nyingine
Bidhaa za Afrika zachanua nchini China huku biashara ya kuvuka mipaka ikiendelea kushamiri
CHANGSHA/NAIROBI - Saa 7 usiku kwa Saa za Nairobi katika shamba la maua la Kenya, wafanyakazi wana shughuli nyingi za kukata waridi zenye sifa bora zaidi duniani, ambazo zina vichwa vikubwa, na ya aina mbalimbali na zinaweza kudumu kwa muda mrefu katika chombo.
Saa moja baadaye, maua hayo ya waridi hupakiwa kwenye lori karibu na Ziwa Naivasha na kisha kuelekea kusini kando ya Bonde la Ufa hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, nchi ambayo ni maarufu duniani kwa kuzalisha maua. Baada ya saa kumi na mbili za kuruka kwa kilomita 8,700 angani, maua hayo yanaingia sokoni katika Mji wa Changsha, Mkoa wa Hunan katikati mwa China baada ya kukamilisha ukaguzi na idhini ya forodha.
Akisubiri kwa hamu maua hayo katika Soko Kuu la Gaoqiao mjini Changsha, Huang Zinan, Mwenyekiti wa Kampuni ya Xiyue Culture Media ya Hunan, mwagizaji wa maua kutoka nje ya nchi, alishusha pumzi baada ya kupata habari kuhusu kibali cha forodha kuruhusu maua hayo kuingia sokoni.
Kuongezeka kujulikana kwa bidhaa za Afrika nchini China
Ukiacha bidhaa za maua kutoka Kenya, kuna bidhaa mbalimbali za Afrika ambazo zimepata kupenya na kukubalika miongoni mwa wateja wa China.
Kuanzia mafuta ya kiwango cha juu ya Madagascar hadi kahawa kutoka Ethiopia, orodha ndefu ya bidhaa za kilimo na chakula za Afrika zenye ubora wa juu zimevutia macho ya wateja wa China na kuamsha hamu yao ya manunuzi.
Kwa mujibu wa takwimu za Idara Kuu ya Forodha ya China, biashara kati ya China na Afrika ilifikia yuan bilioni 822.32 katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.4 mwaka jana wakati kama huo.
Njia rahisi kwa bidhaa za Afrika kuingia China
Msisimko ulijaa hewani wakati masanduku yanayofungisha samaki kutoka Afrika, vilivyohifadhiwa kwa nitrojeni kimiminika, yalipokuwa yakifunguliwa. Juni 20 mwaka huu Soko Kuu la Gaoqiao huko Changsha liliagiza moja kwa moja samaki wabichi wa baharini kutoka Afrika kwa mara ya kwanza, wakiwemo kaa wa bluu kutoka Madagascar na abalone kutoka Afrika Kusini. Kwa jumla, shehena hii ya samaki ilikuwa na uzito wa tani 3.5, ikijumuisha aina 18 tofauti kutoka nchi nne za Afrika.
Su Junping, Rais wa Jumuiya ya Kuhimiza Biashara na Uwekezaji wa Pamoja wa Asia-Ulaya na Afrika, amesema kuwa China imeanzisha kwa ufanisi "njia rahisi" kwa ajili ya uagizaji wa bidhaa za kilimo za Afrika, na idadi kubwa zaidi ya shehena za bidhaa hizo zimeidhinishwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma