Lugha Nyingine
Maonyesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yafunguliwa Changsha (5)
Picha iliyopigwa Juni 29 ikionyesha eneo la maonesho ya Tanzania.(Picha na Song Ge/Tovuti ya Gazeti la Umma) |
Maonesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yamefunguliwa jana Alhamisi huko Changsha, China.
Kaulimbiu ya maonyesho hayo ni "Kutafuta maendeleo kwa pamoja na kunufaika pamoja na siku nzuri za baadaye ". Nchi za Benin, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Madagascar, Malawi, Morocco, Msumbiji, Nigeria na Zambia zimekuwa nchi waheshimiwa katika maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yamevutia kampuni 1,500 kushiriki kwenye maonesho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 70 ikilinganishwa na maonesho hayo ya awamu iliyopita. Bidhaa 1,590 kutoka nchi 29 zilionyeshwa katika maonesho hayo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 165.9 kuliko maonesho hayo yaliyopita.
Habari zinasema kuwa maonesho hayo yatafanyika kutoka Juni 29 hadi Julai 2, siku mbili za kwanza yanafunguliwa kwa watembeleaji wanaoshughulikia biashara husika, na kuanzia Julai 1, yatafunguliwa kwa umma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma