Lugha Nyingine
Magari ya kifahari aina ya SUV kutoka China yavutia wapenzi wa magari wa Saudi Arabia (2)
Picha iliyopigwa Januari 28, 2023 ikionyesha mtembeleaji akipiga picha ndani ya gari la EXEED kwenye maonyesho huko Riyadh, Saudi Arabia. (Wang Haizhou/Xinhua) |
RIYADH – Magari ya kifahari aina ya SUV kutoka China, yaliyokuwa yakioneshwa jukwaani kwenye shughuli iliyofanyika katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh siku ya Jumamosi, yamevutia wapenzi wa magari.
Gari la EXEED VX, ambalo ni bora lenye siti 7, linaleta uzoefu wa kipekee na urefu wa karibu mita 5 na msingi wa gurudumu wenye ukubwa wa karibu mita 3.
Shughuli hiyo pia ilishuhudia kuoneshwa kwa gari la EXEED TXL, aina ya SUV kwa pande zote, pamoja na EXEED LX, ambalo ni gari aina ya SUV ya kompakt lililoundwa mahususi kwa watumiaji vijana wanaofuata mitindo ya kisasa.
Kampuni inayounda magari ya China imesema, Modeli za magari ya EXEED 2023 zimezinduliwa hivi majuzi katika nchi hiyo ya kifalme, zinafaa kwa hali ya hewa ya Saudi Arabia na zina mifumo mipya ya sasa ya ulinzi na usalama.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma