Lugha Nyingine
Kenya yapokea watalii 3,000 waliowasili kwa meli za utalii ndani ya miezi miwili (2)
Watalii wakishuka kutoka kwenye meli ya utalii huko Mombasa, Kenya, Novemba 27, 2022. (Picha na Dihoff Mukoto/Xinhua) |
NAIROBI - Kenya imepokea watalii 3,000 waliowasili kwa meli za utalii za kimataifa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, afisa wa serikali alisema siku ya Alhamisi.
John Ololtuaa, Katibu Mkuu katika Wizara ya Utalii ya Kenya, amesema kuwa Kenya inanufaika kutokana na maendeleo ya miundombinu katika kituo kipya cha meli kilichoboreshwa katika Bandari ya Mombasa ambacho kimesaidia eneo hilo ambalo ni kivutio kwa watalii kuwa sehemu ya utalii wa meli.
"Meli mbili zaidi zinatarajiwa kufika bandarini kabla ya mwisho wa robo hii," Ololtuaa amesema baada ya kupokea wageni 800 na wafanyakazi wa meli ya MV World Odyssey katika Bandari ya Mombasa ya Kenya.
Ololtuaa amesema uendelezaji wa kituo hicho ulikuwa muhimu huku wapangaji zaidi wa usafiri wa meli za utalii sasa wakiilenga Kenya ndani ya ratiba zao.
Pia amesema kuwa kurejea kwa meli ya MV World Odyssey ni ushahidi wa ushawishi wa Kenya kwa wasafiri wa kimataifa.
"Hiki ni ishara ya wazi ya kuongezeka kwa maslahi ya mashirika ya utalii katika eneo letu na hasa ukanda wa pwani ambao ni sehemu muhimu ya bidhaa ya utalii ya Kenya," ameongeza.
Ololtuaa amesema, Kenya soko la usafiri wa meli za utalii litakuwa kama sehemu ya mkakati wa kutangaza na kuendelesha shughuli za utalii nchini humo.
Ameelza kuwa watalii wa meli za utalii ni sehemu muhimu ya shughuli za utalii kutokana na matumizi yao makubwa ambayo yameleta mapato ya ziada muhimu kwa eneo la utalii , na utalii wa meli za utalii ni soko la thamani kubwa ya mabilioni ya dola, haswa kwa maeneo ambayo yamewekeza zaidi kwenye miundombinu husika pamoja na kutangaza maeneo yao duniani kote.
John Chirchir, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Utalii ya Kenya, amesema kuwa kurejea kwa MV World Odyssey nchini Kenya kunaonyesha kuwa eneo hilo lina fursa za utalii zinazomfaa kila mgeni anayefika nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma