Lugha Nyingine
Nchi nyingi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” zashiriki kwenye Maonesho ya Saba ya Bidhaa za Utamaduni ya Sanya (7)
Asubuhi ya Tarehe 30, Disemba, 2022, Maonyesho ya Saba ya Kimataifa ya Bidhaa za Utamaduni ya Sanya yaliyofanyika kwa siku 4 yalifunguliwa kwa shangwe kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Hongshulin mjini Sanya, China, ambapo kampuni kutoka nchi na maeneo 32, na kampuni za utalii na utamaduni zaidi ya 260 kutoka nchini China zimeshiriki pamoja kwenye maonesho hayo, zikionesha bidhaa za utalii na utamaduni zaidi ya 40,000.
Katika mabanda ya nchi na maeneo hayo 32, kuna nchi zimeshiriki zikiwemo Nepal, Yemen, Indonesia, Pakistan, Afghanistan, Iran, Mongolia na nchi nyingine zinazoshiriki kwenye “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Kampuni kutoka sehemu hizo zimetoa bidhaa zao zinazopendwa zaidi, ambazo zilivutia wakazi na watalii kutazama na kununua.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma