Lugha Nyingine
Maisha ya wakazi yarejea kawaida Beijing
Wateja wakiwa kwenye mkahawa katika eneo la Sanlitun, Beijing mchana wa siku ya tarehe 22,. (Mpiga picha: Yukai/Tovuti ya Gazeti la Umma) |
Mfanyakazi wa jumba la sinema amemwaambia wandishi wa habari kuwa kuanzia wiki iliyopita watazamaji wa filamu wameongezeka kidhahiri, haswa tangu Filamu ya "Avatar 2" ilipoanza kuoneshwa nchini China, hata kwa wakati ujao tiketi zote zimeuzwa . "
"Ni muda mrefu sasa, sijaona watu wengi kama hivi, nimesisimka sana." Du Hua, ambaye anafanya uuzaji wa bidhaa katika Kituo cha Reli cha Magharibi cha Beijing, amewaambia waandishi wa habari: "Kulikuwa na muda kabla ya hapo wakati hapakuwa na watu wengi wanaosafiri, kwa jumla kuna vyumba 13 vya abiria kungojea treni kwenye kituo kizima, na ni vyumba 2-3 tu vilifunguliwa, lakini kuanzia siku hizi, vyumba vya abiria kungojea treni vimefunguliwa moja baada ya kingine, na wateja wameongezeka zaidi, na bila shaka hali ya biashara yetu pia imekuwa nzuri.”
Katika siku za hivi karibuni, kutokana na kutolewa mfululizo kwa sera za kuboresha hali ya utekelezaji wa hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona, watu wamepata urahisi katika usafiri, maduka mengi makubwa ya Beijing yametangaza kurejesha hali ya kawaida ya kula kwenye migahawa, ununuzi wa bidhaa mtandaoni umeanza kufufuka kwa kasi. Msongamano mkubwa wa magari na kuongezeka kwa abiria kumeonesha uhai wa mji wa Beijing. Sasa, tufuate kamera ya waandishi wa habari kujionea hali ya kurejea kawaida kwa maisha ya watu iliyopotea kwa muda mrefu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma