Lugha Nyingine
Maonyesho ya Majira ya baridi ya Mazao ya Kilimo ya Kitropiki ya China (Hainan) 2022 yafunguliwa (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2022
Hii ni droni ya kuhifadhi mimea iliyooneshwa kwenye Ukumbi wa kuimarisha Kilimo kwa Sayansi na Teknolojia (picha iliyopigwa Tarehe 5, Desemba). |
Siku hiyo, Maonyesho ya Majira ya baridi ya Mazao ya Kilimo ya Kitropiki ya China (Hainan) 2022 yalifunguliwa katika Kituo cha Mikutano na Maonyesha cha Kimataifa cha Hainan huko Haikou. Eneo la jumla la maonyesho hayo ni mita 70,000 za mraba, ambapo kuna kumbi 10 za maonesho, zikiwemo Ukumbi wa kuimarisha Kilimo kwa Sayansi na Teknolojia, Ukumbi wa kustawisha Vijiji , na Ukumbi wa mazao bora ya nchini na ya Kimataifa. Makampuni 1,200 kutoka mikoa 18 kote nchini yameshiriki kwenye maonyesho hayo, ambapo mazao ya kilimo ya aina 2000 yameoneshwa kwenye maonyesho hayo, yakiwemo pamoja na matunda na mboga, nafaka na mafuta ya kupikia, mazao ya majini, na mifugo. (Mpiga picha: Guo Cheng/Xinhua)
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma