Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping awasili Bali nchini Indonesia kwa ajili ya kushiriki mkutano wa G20 (3)
Rais wa China Xi Jinping akiwasili kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 17 wa Kundi la Nchi 20 duniani (G20) huko Bali, Indonesia, Novemba 14, 2022. (Xinhua/Shen Hong) |
BALI, Indonesia - Rais wa China Xi Jinping amewasili hapa Jumatatu kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 17 wa Kundi la Nchi 20 (G20).
Msafara wa Xi umejumuisha Peng Liyuan, mke wa Xi, Ding Xuexiang, Mjumbe wa Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, na He Lifeng, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na naibu mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Watu wa China.
Alipowasili, Xi alikaribishwa kwa furaha kwenye uwanja wa ndege na maofisa viongozi wa Indonesia, akiwemo Luhut B. Pandjaitan, Mratibu wa Ushirikiano na China na Waziri Mratibu wa Masuala ya Bahari na Uwekezaji, na Gavana wa Bali Wayan Koster.
Askari wa Gwaride la heshima walizunguka zulia jekundu kutoa heshima kwa Xi. Vijana wa Indonesia waliovalia mavazi ya kitaifa walipiga Gamelan, ala ya muziki ya kitamaduni ya Indonesia, huku mabinti wakicheza "ngoma ya Pendet" ya Bali.
Wakipeperusha bendera za Taifa za China na Indonesia, wanafunzi wa huko walishangilia kwa kusema "karibu, karibu" kwa Lugha ya Kichina.
Balozi wa China nchini Indonesia Lu Kang pia aliwakaribisha wajumbe wa msafara kwenye uwanja wa ndege.
Pande mbili za barabara kutoka uwanja wa ndege hadi kwenye hoteli atakayokaa Rais Xi na mkewe, wakazi wengi wa eneo hilo walikusanyika na kupeperusha bendera za nchi hizo mbili ili kumkaribisha kwa furaha Rais wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma