Lugha Nyingine
Kimbunga Nicole chakumba maeneo ya pwani ya Florida, Marekani
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 11, 2022
Novemba 10, Mwaka 2022 kwa saa za huko, nyumba nyingi ziliharibiwa vibaya baada ya Kimbunga Nicole kutokea kwenye Ufukwe wa Daytona, Florida. Kituo cha Kitaifa cha Kimbunga cha Marekani kiliripoti kuwa "Nicole" ilipotokea kwenye Kisiwa cha Grand Bahama saa 11 ya mchana ya Tarehe 9 kwa saa za Mashariki ya Marekani, kasi ya upepo wa juu ilikuwa kilomita 121 kwa saa. Maeneo mengi ya Jimbo la Florida yametoa maonyo ya kimbunga, na umeme umekatika katika makumi ya maelfu ya familia katika maeneo ya pwani ya jimbo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma