Lugha Nyingine
Shenzhen “Mji Mkuu wa Saa wa China” unaochukua asilimia 42 ya uzalishaji wa saa za mkono duniani (2)
Ikiwa moja ya tasnia za jadi za mji wa Shenzhen wa China, tasnia ya uzalishaji saa ya Shenzhen inawakilisha kiwango cha juu zaidi nchini China, na pia ni nguvu muhimu katika tasnia ya mtindo wa fasheni za kisasa wa Shenzhen.
Tasnia ya saa ya Shenzhen ilianza kustawi kutokana na viwanda vya Hong Kong kuanza kuhamia sehemu ya ndani ya China Bara baada ya kuanza kutekelezwa kwa sera ya mageuzi na kufungua mlango. Baada ya kupitia vipindi vya usindikaji nyenzo, kuvumbua bidhaa mpya na kuanzisha chapa, hivi sasa Shenzhen inaongoza kabisa katika sekta hiyo nchini China, na pia inaongoza chapa za saa za China kuingia soko la kimataifa.
Takwimu zinaonesha kuwa, uzalishaji wa saa za mkono wa China unachukua asilimia 80 ya uzalishaji wa jumla duniani, huku saa za mkono zilizozalishwa mjini Shenzhen zinachukua asilimia 53 ya ujumla ya uzalishaji wa China, na asilimia 42 ya ule wa dunia nzima. Bila shaka Shenzhen inastahili kuitwa “Mji Mkuu wa Saa wa China”.
Hivi sasa Shenzhen ina chapa zaidi ya 200 za saa, ambazo zinachukua zaidi ya asilimia 70 ya mauzo ya chapa zote za saa za China. Katika chapa hizo, nyingi zimeingia masoko ya saa ya Ulaya, Mashariki ya Kati, Afrika, Asia ya Kusini Mashariki n.k.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma