Lugha Nyingine
Benki Kuu ya China yasema kiwango cha ukuaji wa uchumi wa China kubaki katika viwango vinavyofaa
Picha kutoka kwenye data ikionyesha jengo la makao makuu ya Benki ya Umma ya China hapa Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Cai Yang)
BEIJING - Kiwango cha ukuaji wa uchumi wa China kinatarajiwa kubaki katika kiwango cha kuridhisha, mkuu wa Benki ya Umma ya China, Yi Gang amesema Jumatano.
Licha ya baadhi ya changamoto na shinikizo la kushuka, uchumi wa China umeendelea kubaki katika mwelekeo mpana, amesema Yi, kwenye Mkutano wa Uwekezaji wa Viongozi wa Mambo ya fedha Duniani ulioandaliwa na Mamlaka ya Fedha ya Hong Kong kwa njia ya video.
Yi amesema sera ya mambo ya fedha ya China inabakia kuunga mkono uchumi halisi, na soko la mambo ya fedha hufanya mgawanyo mzuri wa rasilimali.
“Benki kuu imetumia sera za fedha za kimuundo, kwa kutoa msaada wa kifedha kwa sekta muhimu kama vile kilimo, biashara ndogo na za kati, na maendeleo ya kijani,” Yi amesema.
Ameongeza kuwa Benki ya Umma ya China pia inasaidia uwekezaji katika matumizi ya mtaji na miundombinu, ambayo athari yake itaonekana katika robo ya nne ya mwaka.
“Shukrani kwa misingi mizuri ya muda mrefu ya uchumi wa China, kiwango cha ubadilishaji cha RMB kimeendelea kuwa tulivu kutokana na kuzingatia hali ya kapu la fedha mbalimbali tangu mwanzoni mwa mwaka,” ameeleza Yi.
Kwa mujibu wake, kiwango cha ubadilishaji wa RMB kitaendelea kubaki thabiti katika kiwango kinachokubalika na kinachofaa, kudumisha uwezo wake wa ununuzi na kuweka thamani yake kuwa thabiti.
“Ili kusaidia maendeleo mazuri ya sekta ya nyumba, benki kuu imepunguza viwango vya mikopo ya nyumba, imepunguza malipo, na kuzihimiza benki kuanzisha mpango maalum wa mikopo kwa makampuni yanayojenga nyumba ili kuhakikisha kukamilika kwa miradi ya nyumba ambayo haijakamilika kwa wakati,” Yi amesema.
Uuzaji na ukopeshaji wa sekta ya mali isiyohamishika umeshuhudia uboreshaji mdogo hivi karibuni, amesema, huku akiongeza kuwa chini ya ukuaji wa miji unaoendelea nchini China, soko la nyumba linaweza kufikia kiwango cha chini cha kupata mikopo.
Kwa mujibu wa Yi, Hong Kong itaendelea kuwa kituo muhimu cha mambo ya fedha cha kimataifa, kinachounganisha soko la China Bara na kimataifa.
Amesema uchumi na mfumo wa mambo ya fedha wa Hong Kong umeonyesha ustahimilivu wa kushangaza licha ya usumbufu katika miaka ya hivi karibuni.
“Hong Kong ina uwezo mkubwa katika kuimarisha uhusiano na soko la mambo ya fedha la China Bara, kufadhili na kuwekeza chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, teknolojia za mambo ya fedha na ufadhili wa maendeleo ya kijani” Yi amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma