Lugha Nyingine
Xi Jinping afanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam
BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Rais wa China, Jumatatu amefanya mazungumzo na Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV).
Pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha urafiki wa jadi, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuongeza kuaminiana kisiasa, na kudhibiti ipasavyo tofauti, ili kusukuma mbele ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Vietnam kwenye ngazi mpya katika zama mpya.
Xi amekaribisha ziara rasmi ya Trong nchini China kufuatia Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, na kueleza kuwa amedumisha mawasiliano ya karibu na Trong kwa njia mbalimbali na kufikia makubaliano mengi muhimu ya kuongoza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Vietnam katika miaka ya hivi karibuni. "Makubaliano haya yametekelezwa kikamilifu na matokeo ya kushangaza yamepatikana," amesema.
Katika mkutano huo, Xi amemfahamisha mgeni wake ajenda kuu za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC. Amesema mafanikio ya kihistoria yaliyopatikana kwa ajili ya CPC na China katika zama mpya yanathibitisha kikamilifu kwamba njia ya ujamaa wenye umaalumu China inalingana na hali halisi ya China, inaakisi matakwa ya watu wa China, na inakidhi matakwa ya nyakati.
Akipongeza mafanikio ya upande wa Vietnam katika ujenzi na uvumbuzi wa kijamaa, Xi amesema inaaminika kuwa chini ya uongozi wa Kamati Kuu ya CPV inayoongozwa na Katibu Mkuu Nguyen Phu Trong, CPV na Serikali ya Vietnam hakika itatimiza malengo na majukumu yaliyowekwa. na Mkutano Mkuu wa 13 wa CPV.
Xi amesema, kutokana na mabadiliko ya kasi ya hali ambayo hayajapata kuonekana katika karne moja iliyopita, Dunia imeingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko. Amesisitiza kuwa China, Vietnam na nchi nyingine za kijamaa zimefanikiwa kufuata mwenendo wa zama na kuchunguza njia ya kisasa inayoendana na hali halisi za nchi zao , na ujamaa unazidi kuwa na nguvu zaidi.
Katika kuendeleza zaidi uhusiano wa China na Vietnam, Xi amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kuzingatia mwelekeo wa ujamaa. "Kwa lengo kuu la ujamaa na uhusiano wa China na Vietnam, kuzingatia mwelekeo sahihi wa kisiasa ni muhimu."
Ameelezea matumaini kuwa pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu na kubadilishana mawazo kuhusu masuala makuu yanayohusu uhusiano baina ya nchi hizo mbili kwa wakati.
Kuhusu uhusiano na Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN), Xi amesema kwamba China pia iko tayari kushirikiana na ASEAN kutekeleza mfumo wa kweli wa uhusiano wa pande nyingi na uwazi wa kikanda, kufanya hali ya kikanda na utaratibu wa kimataifa kuwa wa amani, wenye utulivu, haki na usawa, na kuhimiza kikamilifu ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Kwa upande wake, Trong amemshukuru Xi kwa kumwalika kuwaongoza viongozi wa Vietnam ikiwa ni wajumbe wa kwanza wa ngazi ya uongozi wa nchi kuzuru China tangu Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC. Trong amesema pia ametimiza ahadi yake ya kuifanya China kuwa nchi yake ya kwanza kutembelea nje ya nchi baada ya kuchaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPV.
Trong amesema Mkutano Mkuu wa 13 wa CPV na ule wa 20 wa CPC ni mwanzo wa hatua mpya muhimu ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili, na Vietnam iko tayari kushirikiana na China kusukuma urafiki wa ujirani mwema baina ya nchi hizo mbili na ushirikiano wa kina wa kimkakati kufikia ngazi mpya ya juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma