Lugha Nyingine
Moduli ya maabara ya kituo cha anga ya juu cha China Mengtian yakamilika, tayari kurushwa kwenye anga ya juu (3)
WENCHANG - Kwa pamoja, moduli ya maabara ya kituo cha anga za juu cha China, Mengtian na roketi yake ya kubebea ya Long March-5B Y4 vimesafirishwa hadi eneo la urushaji, Idara ya Safari ya Anga ya Juu ya China imesema Jumanne.
Moduli ya maabara itatumwa kwenye obiti kwa wakati unaofaa katika siku za usoni. Kabla ya urushaji wake, ukaguzi wa ufanisi na majaribio ya pamoja yatafanywa kama ilivyopangwa.
Mitambo na vifaa katika Eneo la Urushaji Vyombo kwenye Anga ya Juu la Wenchang katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China viko katika hali nzuri, na idara zote zinazohusika na ujumbe huo zinaendelea na maandalizi ya mwisho, shirika hilo limesema katika taarifa yake.
Vifaa vya kisayansi katika moduli ya Mengtian, sehemu ya pili ya maabara ya kituo cha anga ya juu cha China, vitatumika kwa ajili ya kuchunguza maikrograviti na kufanya majaribio ya fizikia ya maji, sayansi ya vifaa, sayansi ya mwako na fizikia ya kimsingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma