Lugha Nyingine
Barabara ya Daraja la Crimean larudia katika hali ya kupita kwa magari
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2022
Shirika la habari la Russia RT tarehe 8 lilinukuu maneno aliyosema ofisa wa eneo la Crimean Sergey Aksyonov likiripoti kuwa, barabara ya Daraja la Crimean limerudi kwenye hali ya kupita kwa magari.
Mapema siku hiyo, lori moja lililipuka kwenye barabara ya Daraja la Crimean, likisababisha kuwaka kwa matangi 7 ya mafuta yaliyobebwa na treni ya mizigo iliyoendeshwa kwenye reli iliyo sambamba na barabara hiyo; sehemu ya barabara iliharibiwa.
Kamati ya uchunguzi ya Shirikisho la Russia ilisema, uchunguzi wa hatua ya kwanza unaonesha kuwa, ajali hiyo imesababisha vifo vya watu watatu. Wachunguzi wamethibitisha kuwa mmiliki wa lori hilo ni mkazi wa eneo la mpaka la Krasnodar la Kusini mwa Russia. Uchunguzi husika bado unaendelea.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma