Lugha Nyingine
DEA yasema gesi ya mabomba ya Nord Stream itaendelea kuvuja hadi Jumapili
Picha iliyopigwa Septemba 27, 2022 ikionesha sehemu ya kuvuja kwa gesi ya mabomba ya Nord Stream. (Picha/CFP)
Mkurugenzi wa Idara ya nishati ya Denmark (DEA) Kristoffer Bottzauw Jumatano ya wiki hii alisema, gesi asilia ya mabomba ya Nord Stream itaendelea kuvuja hadi mwishoni mwa wiki hii.
“Tunakadiria gesi ya mabomba itaendelea kuvuja hadi mwishoni mwa wiki hii. Bado kiasi kikubwa cha gesi asilia zinavuja kutoka kwenye sehemu tatu zenye tundu au ufa. Inaonekana kama shinikizo ndani ya mabomba linashuka, kwa hivyo gesi iliyovuja imepungua ikilinganishwa na jana. Tunatumai hali hii itaonekana pia katika siku zijazo,” lilisema shirika la habari la Denmark Ritzau likinukuu maneno ya Bottzauw.
“Halafu, kuanzia upande wa Denmark, tutafanya uchunguzi juu ya sababu za kuvuja kwa gesi na kukaribia mabomba hayo, ili tuweze kufanya uchunguzi kikamilifu .”
Jumatatu ya wiki hii, ripoti husika zilisema kuwa, matukio matatu ya kuvuja kwa gesi ya mabomba ya Nord Stream 1 na 2 yalitokea kwenye eneo la bahari la kimataifa. Kati ya matukio hayo matatu, mawili yalitokea kwenye eneo la kiuchumi la Denmark, na lingine lilitokea kwenye eneo la kiuchumi la Sweden.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma