Lugha Nyingine
Wimbi la matumizi wakati wa likizo laonesha uwezo wa ongezeko la soko la China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2022
Wateja wakinunua vitu kwenye kituo cha maduka huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong wa Kusini mwa China. (Xinhua/Huang Guobao)
Likizo ya Sikukuu ya Taifa ya China kuanzia tarehe 1 hadi 7, Oktoba ilikuwa msimu wa matumizi makubwa. Mwaka huu serikali ilitoa sera mbalimbali za kuhimiza matumizi kabla ya likizo hiyo.
Takwimu za wizara ya utamaduni na utalii zilizotolewa Ijumaa ya wiki iliyopita zimeonesha kuwa, katika wakati wa likizo hiyo ya mwaka huu, idadi ya watalii ilifikia milioni 422 hivi nchini China.
Takwimu hizo pia zimeonesha kuwa, mapato ya jumla ya shughuli za utalii nchini China katika wakati wa likizo yamefikia Yuan bilioni 287.2 (sawa na Dola za Marekani bilioni 40.5).
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma