久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa yakuza uchumi wakati ambapo China inaendelea kufungua mlango kwa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 06, 2022

SHANGHAI - Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), yanayotarajiwa kufanyika mwezi mmoja kutoka sasa, yako katika hatua ya mwisho ya maandalizi huku makampuni ya kigeni yakitarajia kutoa fursa za masoko.

Maonyesho hayo, yatakayofanyika katika kitovu cha uchumi cha China, Shanghai, yamepangwa kufanyika licha ya athari za janga la UVIKO-19, na yanaonyesha dhamira ya nchi ya China ya kufungua zaidi soko lake kubwa kwa ukuaji wa pamoja wa uchumi wa Dunia.

Picha iliyopigwa Oktoba 5, 2021 ikionyesha usakinishaji wa mapambo karibu na Kituo cha Taifa cha Maonyesho na Mikutano cha Shanghai, ambacho ni eneo kuu la Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE), Mjini Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)

Maandalizi ya mwisho

Kadri Maonyesho ya Tano ya CIIE yanapokaribia, washiriki na bidhaa zao wanaendelea kuwasili Shanghai kupitia njia mbalimbali. Septemba 20, shehena ya kwanza ya bidhaa kutoka nje ya China, yenye thamani iliyotangazwa ya Yuan milioni 560 (kama dola za Kimarekani milioni 78.7), ilitolewa kwenye forodha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pudong wa Shanghai.

Picha iliyopigwa Oktoba 22, 2021 ikionyesha mapambo yaliyowekwa karibu na lango la Kituo cha Taifa cha Maonyesho na Mikutano cha Shanghai, eneo kuu la Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China (CIIE), katika Mji wa Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)

Treni ya mizigo ya kati ya China na Ulaya pia imekuwa chaguo maarufu la usafiri miongoni mwa makampuni yanayoshiriki CIIE, anasema Wang Jinqiu, Mwenyekiti wa Kampuni ya Usafirishaji ya Shanghai Oriental Silk Road huku akiongeza kuwa huu ni mwaka wa pili wa huduma hiyo kuwasilisha bidhaa kwenye CIIE huko Shanghai.

Kwa mujibu wa Forodha ya Shanghai, mwisho wa kuwasili kwa bidhaa zitakazooneshwa kwenye maonyesho hayo ni mwezi huu wa Oktoba. Forodha ya Shanghai imesema itaendelea kuboresha mchakato wa uidhinishaji wa bidhaa hizo za maonyesho na kutoa huduma salama, rahisi na bora za vibali vya forodha.

Sun Chenghai, Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya CIIE amesema kazi ya kualika makampuni ya biashara kushiriki katika CIIE ya tano imekamilika na maendeleo chanya yanafanywa katika kupanga maonyesho.

Fursa za Biashara

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya makampuni 280 kati ya makampuni 500 bora duniani na makampuni makubwa ya viwanda yatashiriki katika CIIE ya mwaka huu, huku karibu asilimia 90 ya washiriki wa mwaka jana pia wakijiunga mwaka huu.

Will Song, makamu mkuu duniani na mwenyekiti wa kampuni ya Johnson & Johnson nchini China, amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita kampuni hiyo imeleta bidhaa mpya mbalimbali kwenye CIIE kila mwaka, na mwaka huu katika maonyesho ya tano, itatambulisha takriban bidhaa 40 mpya.

Naibu Waziri wa Biashara wa China Sheng Qiuping anasema CIIE imetoa mchango kamili katika jukumu lake kama dirisha la kujenga jukwaa la ushirikiano kwa wale wanaohusika ndani na nje ya China, na imekuwa mahali pa waonyeshaji kuonyesha bidhaa zao mpya za kimataifa, teknolojia ya hali ya juu na huduma za ubunifu.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Biashara ya China, kuanzia Mwaka 2018 hadi 2021, waonyeshaji katika awamu nne za awali za CIIE walizindua bidhaa, teknolojia na huduma mpya zaidi ya 1,500, na mauzo yaliyokusudiwa yanayozidi dola bilioni 270 za Marekani.

Muonyeshaji bidhaa (wa pili kushoto, mbele) akijadiliana na wanunuzi watarajiwa wakati wakishiriki mkutano wa kutambulishana wa ugavi wa awali wa mahitaji wa kabla ya maonyesho kwa ajili ya Eneo la Maonyesho ya Viwanda vinavyotumia Akili Bandia na TEHAMA la Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) katika Kituo cha Taifa cha Maonyesho na Mikutano cha Shanghai, Mashariki mwa China, Agosti 8, 2022. (Xinhua/Fang Zhe)

Kuaminika kwa soko

CIIE inaonyesha dhamira thabiti ya China ya kufungua mlango, ambayo imeongeza imani ya makampuni mengi ya kigeni.

"Licha ya kutokuwa na uhakika wa mazingira ya kimataifa, CIIE itafanyika nje ya mtandao kama ilivyopangwa. Ni aina hii ya uhakika ambayo inaipa Dunia imani hata zaidi katika uhakika na azma ya China ya kukua kiuchumi pamoja na washirika wake wa kimataifa," amesema Pietro Brambilla, Afisa Mkuu wa Fedha wa L'Oreal Eneo la Asia Kaskazini na China. 

Watu wakijadiliana wakati wakishiriki mkutano wa kutambulishana wa ugavi wa awali wa mahitaji wa kabla ya maonyesho kwa ajili ya Eneo la Maonyesho ya Viwanda vinavyotumia Akili Bandia na TEHAMA la Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) katika Kituo cha Taifa cha Maonyesho na Mikutano cha Shanghai, Mashariki mwa China, Agosti 8, 2022. (Xinhua/Fang Zhe)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>