Lugha Nyingine
Maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China 2022 yafanyika Beijing
Picha iliyopigwa tarehe 29, Agosti ikionesha muonekano nje ya Jumba la Huduma za mawasiliano ya simu, Kompyuta na Upashanaji wa Habari la Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China kwenye eneo la Bustani ya Shougang. (Picha ilipigwa na Han Xu/Xinhua)
Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China 2022 yalifunguliwa Beijing Jumatano ya wiki hii.
Maonesho ya mwaka huu yatafanyika hadi tarehe 5, Septemba, yakihusisha mkutano wa kilele wa biashara ya huduma ya dunia, maonesho, mabaraza, matangazo ya bidhaa mpya na teknolojia mpya, majadiliano ya biashara na shughuli nyingine kadha wa kadha.
Maonesho hayo yalianzishwa mwaka 2012, na mwaka huu, eneo maalumu la huduma ya mazingira limewekwa kwa mara ya kwanza kwenye maonesho hayo.
Maonesho hayo yanaendelea kukua katika muongo uliopita, na yamekuwa moja ya majukwaa matatu makuu ya China kwa kuhimiza kufungua mlango na ushirikiano wa kimataifa.
Maonesho ya mwaka huu yatakuwa ya kimataifa zaidi, ambapo kampuni zaidi ya 2400 yameshiriki kwenye maonesho hayo, zikiwemo kampuni karibu 400 ambazo ni za kati ya kampuni 500 bora duniani au kampuni za kuongoza sekta zao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma