Lugha Nyingine
Benki ya NCBA ya Kenya kushirikiana na Kampuni ya Huawei kutoa huduma za benki kidijitali
NAIROBI- Shirika la Huduma za Kifedha la Kenya NCBA Jumatatu wiki hii limesema kuwa linashirikiana na kampuni ya teknolojia ya China, Huawei ili kutoa huduma za benki kidijitali kwa wateja wake.
John Gachora, Mkurugenzi Mkuu wa NCBA, amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi, Kenya, kwamba kampuni hiyo ya China ina uwezo wa kutengeneza programu za simu za kidijitali zinazoruhusu miamala ya kifedha kufanyika kati ya fedha za Kenya na fedha nyingi za kigeni.
"Ushirikiano wetu utatengeneza benki ya kidijitali yenye mfumo wa malipo wa kimataifa unaolenga kuboresha uzoefu mzuri kwa wateja," Gachora amesema wakati NCBA ilipotoa ripoti yake ya nusu mwaka ya kifedha inayoishia Juni 30.
NCBA kwa sasa inatoa huduma za kibenki nchini Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda na Cote d'Ivoire.
Gachora amesema kuwa NCBA itaharakisha mchakato wake kuelekea benki ya kidijitali kwa sababu utaiwezesha benki hiyo kuimarisha ufanisi wake kwa kuwapa fursa wateja kupata huduma za kifedha wakati wowote na mahali popote. Ameelezea imani yake kuwa matumizi ya kidijitali pia yataongeza uwezo wa benki hiyo kuhudumia jamii inayokua ya Wachina katika Afrika Mashariki kwa kutoa suluhu ya miamala ya kifedha kati ya Afrika Mashariki na China bila vikwazo.
NCBA tayari inaunga mkono idadi kadhaa ya makampuni ya China yanayotekeleza miradi ya miundombinu katika eneo la Afrika Mashariki kupitia bidhaa za kifedha kwenye kibiashara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma