Lugha Nyingine
Rais wa China atoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Pakistan kufuatia maafa makubwa ya mafuriko nchini Pakistan
(CRI Online) Agosti 30, 2022
Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Pakistan Bw. Arif Alvi kutokana na maafa makubwa ya mafuriko nchini Pakistan.
Rais Xi amesisitiza kuwa, kwa niaba yake na serikali ya China na watu wake pamoja, anatoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga.
Amesema, baada ya maafa hayo kutokea, China ilichukua hatua mara moja ya kutoa misaada inayohitajika, na kwamba China itaendelea kutoa msaada unaohitajika kwa Pakistan ili kuisaidia kukabiliana na maafa.
Pia waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Pakistan Bw. Shahbaz Sharif kufuatia maafa hayo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma