Lugha Nyingine
Magari ya nishati mpya ya China yaongoza soko la kimataifa (2)
Watu wakitembelea eneo la BYD katika maonesho ya magari bora yasiyochafua mazingira ya mwaka 2022 yaliyofanyika California, Marekani, Mei 10. (Picha/Xinhua) |
Takwimu zilizotolewa siku hizi na kampuni ya BYD zinaonesha, uuzaji wa magari yanayotumia nishati mpya wa kampuni hiyo katika nusu ya kwanza ya mwaka huu umezidi laki 6.4. Hali hiyo inamaanisha BYD imeshinda Tesla na kuwa kampuni ya uundaji wa magari ya nishati mpya ambayo uuzaji wake ni mkubwa zaidi duniani.
Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni za magari za China zinapanua soko lake nje ya nchi kwa hatua madhubuti kwa kutegemea nguvu yake halisi. Kutoka Ulaya hadi Mashariki ya Kati na Lating Amerika, magari ya nishati mpya ya China yamenunuliwa vizuri katika nchi nyingi zaidi, na siyo tu yamehimiza hali ya kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa gesi katika nchi hizo, bali pia yametoa fursa kwa mawasiliano kati ya viwanda vyao vya magari.
Baada ya BYD kuanzisha kampuni yake ndogo nchini Uingereza mwaka 2012, kampuni hii ilishirikiana na kampuni ya mabasi ya Alexander Dennis (ADL) ya nchi hiyo, ambapo zimeleta bidhaa zenye uvumbuzi kwa nchi hiyo na nchi nyingine. Meneja mkuu wa kampuni ya ADL Paul Davies alisema, kampuni ya ADL na ya BYD zilishirikiana kuunda mabasi zaidi ya 1000 kwa soko la Uingereza kuanzia mwaka 2016; na kiasi hicho kinatazamiwa kuzidi 1500.
Wadau wengi wanaona kuwa, viwanda vya magari ya nishati mpya vya China vinaendelea kwa kasi, na nguvu yake ya ushindani inazidi kuwa kubwa siku hadi siku. Kampuni za China zinaelekea kipindi kipya cha fursa ya kihistoria katika mashindano ya kuunda magari ya nishati mpya.
Bustani ya Wanyama ya Chongqing yawasaidia wanyama kuepuka joto
Watu wafuruhia hali ya hewa nzuri wakati wa majira ya joto kwenye sehemu ya Mto Wujiang, Chongqing
Bwawa la Sanmenxia la katikati mwa China laanza kufanya kazi ya Kuondoa tope la mchanga
Mandhari ya Ziwa Yamdrok katika Mji wa Shannan, Mkoa wa Tibet, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma