Lugha Nyingine
Rais Xi wa China akagua Mji wa Wuhan, asisitiza uvumbuzi wa kisayansi, udhibiti wa UVIKO-19, usimamizi wa kijamii (3)
Rais wa China Xi Jinping akitembelea karakana ya Kampuni ya Uhandisi ya HGLaser huko Wuhan, Juni 28, 2022. (Xinhua/Ju Peng) |
WUHAN - Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kujenga nguvu za China katika sekta ya sayansi na teknolojia, kufuata sera ya maambukizi sifuri ya UVIKO na kuboresha usimamizi wa kijamii.
Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati kuu ya Kijeshi ya China, ameyasema hayo alipofanya ukaguzi wake huko Wuhan, Mji Mkuu wa Mkoa wa Hubei katikati mwa China, Jumanne wiki hii.
Xi amesisitiza haja ya kuhimiza zaidi teknolojia na sekta za hali ya juu zaidi, kupanua nyanja mpya za maendeleo ya kiuchumi, na kutengeneza uwezo mpya wa kufanya ushindani duniani.
Alipotembelea Kampuni ya Uhandisi ya HGLaser Xi amehimiza juhudi za kuimarisha utafiti na maendeleo ya teknolojia husika, kumiliki teknolojia za msingi zaidi zenye haki miliki ya kujitegemea, kupanua minyororo ya uvumbuzi, na kuboresha minyororo ya viwanda.
Kisha Xi alitembelea jumuiya ya makazi iitwayo Zhiyuan katika Eneo la Maendeleo ya Teknolojia ya Juu la Ziwa la Wuhan Mashariki.
Katika eneo hilo Xi alisema kuwa Wuhan imedhibiti haraka maambukizi ya UVIKO-19 yaliyotokea katika maeneo kadhaa ya mji huo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita tangu mji huo ushinde vita dhidi ya milipuko hiyo Mwaka 2020.
“Hii inaonyesha kwamba hatua za kukabiliana na janga zilizowekwa na Kamati Kuu ya CPC ni sahihi na zinafaa, ni lazima zishikiliwe bila kuyumbayumba,” Xi amebainisha.
Xi amesema, jamii inabeba jukumu muhimu sana, iwe katika kukabiliana na janga la dharura au kwenye nyakati za kawaida za kuzuia na kudhibiti janga.
Akihimiza uboreshaji wa mbinu za kuzuia na kudhibiti UVIKO-19 unaozingatia jamii mara kwa mara, Xi amesisitiza kuchukua hatua madhubuti, zenye msingi wa kisayansi na kali katika ngazi ya jamii wakati maambukizi mapya yanapogunduliwa.
Akizungumzia mapambano ya jumla ya nchi hiyo dhidi ya UVIKO-19, Xi amesema hatua za China za kukabiliana na mlipuko huo zimelinda maisha na afya ya watu kwa kiwango kikubwa zaidi.
Amesema, iwapo China ingepitisha sera ya "kinga ya jamii" au mbinu ya kutochukua hatua, kwa kuzingatia idadi kubwa ya watu, nchi hiyo ingekabiliwa na matokeo yasiyoweza kufikiria.
"Ikiwa tutafanya tathmini ya jumla, hatua zetu za kukabiliana na UVIKO-19 ndizo za kiuchumi na zenye ufanisi zaidi," amesema.
Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China chini ya Xi ilitangaza kutekeleza sera ya maambukizi sifuri ya UVIKO ambayo huzingatia kuchukua hatua kali, za haraka na za kupima kwa wingi watu pale maambukizi yanapobainika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma