Lugha Nyingine
Ziwa Lugu la mwanzoni mwa majira ya joto lapendazwa kama “kioo mbinguni ” (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2022
Ziwa Lugu la mwanzoni mwa majira ya joto likipendezwa kama “kioo mbinguni”. (Mpiga picha: Cai Shujing/Tovuti ya Gazeti la Umma) |
Mei 14, jua lilitokea baada ya kunyesha mvua katika Ziwa Lugu lililoko kwenye makutano ya mpaka wa Mkoa wa Sichuan na Mkoa wa Yunnan, ambapo mawingu meupe ni kama yanayoelea kwenye maji.
Ziwa Lugu ni ziwa la tatu la maji safi kwenye uwanda wa juu katika nchi yetu, na sifa ya maji ya ziwa hilo inadumu kuwa ya Daraja la kwanza. Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Lijiang mkoani Yunnan umefanya juhudi kubwa za kutekeleza hatua za kujenga mikanda ya ikolojia ya kando ya ziwa, kurejesha ardhi oevu ya ikolojia, na kushughulikia hali ya kiikolojia katika mito inayoingia ziwani, ili maji ya ziwa hilo lililo kama lulu ya uwanda wa juu yawe safi daima.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma