Lugha Nyingine
Msanii wa Hebei, China atengeneza sanaa za uchongaji kwenye magamba ya mayai (5)
(Picha ilipigwa na Lv Minghui/Chinanews) |
Ili kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China, msanii wa Mkoa wa Hebei, China Huo Guangjian alitengeneza Sanaa za mfululizo za uchongaji kwenye magamba ya mayai zinazoitwa “Dong’ao” (neno la Kichina, maana yake ni Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi) na “Fu’hu” (maana yake ni chuimilia anayeleta Baraka). Msanii huyu akitengeneza Sanaa hizo kwa kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China wa chuimilia kwa kalenda ya kilimo ya China, huku akieleza matarajio yake kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na kutumai michezo hiyo ipate mafanikio mazuri.
Sanaa hii ya uchongaji kwenye magamba ya mayai ni Sanaa ya mikono ya kienyeji katika sehemu mbalimbali nchini China. Sanaa hiyo inatengenezwa kwa kutumia mayai ya kuku au mbuni kwa kupitia ustadi mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma