Lugha Nyingine
Mwenge, medali na wimbo rasmi wa Michezo ya Majira ya Baridi ya Asia vyazinduliwa
Picha hii inaonyesha mwenge wa Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China. (Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia/kupitia Xinhua)
HARBIN - Mwenge, medali na wimbo rasmi wa Michezo ya Majira ya Baridi ya Asia Mwaka 2025 itakayofanyika Harbin, Mkoani Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China vimezinduliwa rasmi jana Jumatano.
Urefu wa mwenge huo ni milimita 735, ukiwa na kipenyo cha juu cha milimita 115 na kipenyo cha kitako cha milimita 50. Maudhui ya muundo, "Ongezeko Kubwa" (kwa kiingereza “Surging”), yanalenga kuonyesha nguvu ya hamasa na shamrashamra ya maisha kwenye mazingira ya asili.
Muundo wa jumla wa mwenge huo unajumuisha vipengele vya uzuri vya kimataifa vikichanganya sanaa ya jadi na ya kisasa ya China.
Muundo wake una umbo la ua la lilaki linalochanua, ukijumuisha rangi kama vile nyekundu, zambarau, na Nyeupe, ikiashiria uaminifu, ukarimu, uwazi, na ujumuishi wa Mkoa wa Heilongjiang na sifa maaulum za mji huo mwenyeji, Harbin.
Medali za Michezo hiyo, iliyopewa jina la "Moyo wa Kasi", pia zimeoneshwa kwa umma siku hiyo. Sehemu za mbele za medali zinachanganya umbo lililopangwa vema la njia ya mashindano ya mbio ikiwa na nembo ya Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia, ikichukua mjongeo wa nguvu na wa kupendeza wa wanamichezo wakicheza.
Wimbo rasmi wa Michezo hiyo unaitwa "Theluji ya Harbin", umepangwa na mtunzi wa nyimbo na mwongozaji Wang Pingjiu na kutungwa na mtayarishaji mashuhuri wa muziki wa China Chang Shilei.
Mashairi na vionjo vya wimbo huo vinaonyesha maono ya umoja, urafiki, na dhamira ya pamoja ya amani na maendeleo miongoni mwa watu wa nchi na maeneo ya Asia, wakifanya kazi pamoja kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.?
Picha hii inaonyesha sehemu za mbele za medali za Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China. (Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia/kupitia Xinhua)
Picha hii inaonyesha sehemu za nyuma za medali za Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia mjini Harbin, Mkoani Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China. (Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya 9 ya Majira ya Baridi ya Asia/kupitia Xinhua)
Kazi ya utafiti wa kisayansi wa fani mbalimbali yakamilika mkoani Xinjiang, China
Mandhari ya majira ya mpukutiko ya Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Huaxi huko Guiyang, China
Barabara Kuu ya Jianhe-Liping yafunguliwa kwa matumizi ya umma kusini magharibi mwa China
Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma