Lugha Nyingine
Tarafa ya Yumai katika Mkoa wa Xizang wa China yafungua ukurasa mpya (9)
Picha ya droni iliyopigwa tarehe 14 Oktoba 2024 ikionyesha mwonekano wa Tarafa ya Yumai ya Mji wa Shannan, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua/Ding Ting) |
Tarafa ya Yumai iko kwenye sehemu ya kusini ya safu za milima ya Himalaya, tarafa hiyo ilikuwa na wakazi watatu tu. Leo hii, tarafa hiyo imekuwa na wakazi zaidi ya 200 na inasimamia vijiji viwili.
Tangu Mwaka 2018, tarafa hiyo ilianza kazi ya ujenzi wa kijiji cha mpakani chenye ustawi ambapo kuna nyumba zenye fremu za chuma, mifereji ya maji, shule, na bustani kuu vikijitokeza moja baada ya nyingine. Mwaka 2019, uwekezaji wa serikali wa yuan zaidi ya milioni 500 (dola za Kimarekani kama milioni 70.28) ulikamilisha ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 50 inayounganisha hiyo na nyingine ya jirani, hali ambayo ilimaliza maumivu yake ya kufunikwa na theluji kila mwaka. Zaidi ya hayo, Shirika la Gridi ya Kiaifa la China lilirefusha njia ya kusambaza umeme wa kilovolti 10 hadi Yumai, ikitoa umeme thabiti na salama.
Mwaka 2023, wastani wa mapato ya kila mwaka ya kila mkazi katika tarafa hiyo ya Yumai ulifikia yuan zaidi ya 40,000 (dola za Kimarekani kama 5,622.08) na eneo la makazi la kila mtu limefikia mita za mraba 40.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma