Lugha Nyingine
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yafanya mazishi ya waliokufamaji?kwenye?ajali?ya feri?iliyotokea?hivi karibuni (3)
GOMA, DR Congo - Mazishi rasmi yamefanyika jana Alhamisi mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuwakumbuka watu waliokufamaji kwenye ajali mbaya ya feri iliyotokea hivi karibuni katika Ziwa Kivu.
Mazishi ya miili 11 iliyotambuliwa ya wakazi wa Goma waliofariki baada ya feri ya "MV MERDI" kupinduka katika Ziwa Kivu wiki moja iliyopita yamefanyika kwenye makaburi ya Makao. Watu takriban 87 walifariki Alhamisi wiki iliyopita baada ya feri hiyo kupinduka karibu na bandari ya Kituku, kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya jimbo hilo ambayo haikutaja idadi ya watu waliokuwemo.
Feri hiyo ilivunjika vipande vitatu na kwa sasa kiko kwenye kina kirefu cha mita takriban 198 katika Ziwa Kivu, amesema Makamu wa Gavana wa jimbo hilo Jean Romuald Lipopo ambaye alikuwepo kwenye mazishi hayo, akibainisha kuwa gesi ya methane katika Ziwa Kivu imekwamisha juhudi za msako.
Feri hiyo iliyokukwa ikitoka Minova katika Jimbo la Kivu Kusini, ilizama kwenye umbali wa mamia ya mita kutoka bandarini baada ya kushindwa kustahimili kasi ya wimbi kubwa, vyanzo vya habari katika bandari ya Kituku vimeeleza. Vyanzo hivyo vya eneo hilo vimeripoti kuwa feri hiyo ilibeba "mzigo mkubwa kupita kisai”.
Njia ya nchi kavu kati ya Goma na Minova imekatika kwa miezi kadhaa kutokana na uhasama kati ya makundi yenye silaha na wanajeshi wa DRC. Matukio ya ajali za meli zilirekodiwa mara kwa mara kwenye Ziwa Kivu kutokana na upepo mkali na kubeba mizigo kupita kiasi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma