久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Wamsumbiji wapigia kura kuchagua viongozi wapya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 10, 2024
Wamsumbiji wapigia kura kuchagua viongozi wapya
Ossufo Momade (mbele) mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji Renamo akionekana baada ya kupiga kura katika kituo kilichoko Maputo, Msumbiji, Oktoba 9, 2024. (Picha na Israel Zefanias/Xinhua)

MAPUTO - Wamsumbiji wameanza kupiga kura siku ya Jumatano ili kuchagua rais mpya ambapo watu takriban milioni 17 wamejiandikisha kupiga kura, wakiwemo wapiga kura 333,839 waliojiandikisha katika diaspora wakishiriki kutoka nchi saba za Afrika na mbili za Ulaya ikiwa ni sehemu ya mchakato wa uchaguzi wa kimataifa wa Msumbiji.

Uchaguzi huo mkuu wa Mwaka 2024 ni uchaguzi wa saba wa urais, huku mgombea wa chama tawala cha Frelimo, Daniel Chapo, mwenye umri wa miaka 47, akilenga kuchukua nafasi ya Rais aliyeko madarakani Filipe Nyusi, ambaye anamaliza mihula yake miwili.

Chapo anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wagombea wengine watatu: Lutero Simango wa chama cha Vuguvugu la Kidemokrasia la Msumbiji, Ossufo Momade wa chama kikuu cha upinzani Renamo, na mgombea huru Venancio Mondlane anayeungwa mkono na Chama cha Matumaini kwa Maendeleo ya Msumbiji.

Mbali na kuchagua rais, wapiga kura pia watachagua wabunge 250 wa Bunge la Taifa na wajumbe 794 wa mabaraza ya majimbo, huku vyama vya siasa 35 vikichuana kuwania viti vya bunge la taifa na vyama na vikundi vya kiraia 14 vikiwania nafasi za majimbo.

Waangalizi kutoka mashirika ya kitaifa na kimataifa wanasema kuwa, mchakato huo wa siku moja wa uchaguzi ulikuwa ukiendelea vizuri huku ripoti zikionyesha kuwa asilimia 92.8 ya vituo 3,297 vilivyotembelewa na waangalizi 800 vilikuwa na uwepo wa wajumbe wa vyama.

Baada ya kupiga kura yake majira ya saa 7:05 asubuhi kwa saa za Msumbiji siku ya Jumatano kwenye Shule ya Sekondari ya Josina Machel mjini Maputo, Rais Nyusi ametoa mwito wa kujizuia wakati wote wa upigaji kura.

"Mchezo una dakika 90. Ni baada tu ya filimbi ya mwisho ndipo tunajua matokeo. Ni lazima tuepuke kutangaza ushindi kabla ya wakati, baada ya dakika 15 au 20, au hata wakati wa mapumziko," amesema, akisisitiza kwamba matokeo hayapaswi kutangazwa kabla ya tamati rasmi.

Shughuli ya kuhesabu kura inatarajiwa kuanza mara baada ya upigaji kura kumaliza. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE) ina siku zisizidi 15 kutangaza matokeo kamili kwa Baraza la Katiba ili kuthibitishwa na kutangazwa rasmi.

Kwa mujibu wa CNE, mchakato wa uchaguzi unafuatiliwa na waangalizi wa kitaifa 11,516 na waangalizi wa kimataifa 412, wakiwemo wajumbe kutoka Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Lugha ya Kireno, Umoja wa Ulaya, na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>