Lugha Nyingine
Wabunge nchini Kenya wapiga kura ya kutokuwa na imani na Makamu wa Rais
Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amepigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na Bunge la Kenya licha ya kujitetea dhidi ya mashtaka ya ukiukaji katiba yaliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Kibwezi Magharibi nchini humo, Mwengi Mutuse.
Kwenye kura hiyo ya kutokuwa na imani iliyopigwa jana Jumanne jioni, wabunge 281 kati ya 349 walipiga kura ya ndiyo kuunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na naibu huyo wa Rais, ikiwa ni miaka miwili tu tangu asaidie kuunda serikali ya Kenya Kwanza katika uchaguzi mkuu wa 2022.
Kwenye zoezi hilo, wabunge 44 walipiga kura ya hapana huku mbunge mmoja akijizuia kupiga kura.
Gachagua amekua Naibu wa Rais wa kwanza katika historia ya Kenya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, akidaiwa kuhusika na tuhuma mbalimbali, ikiwemo kujilimbikizia mali na uchochezi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma