Lugha Nyingine
Msemaji wa China asema: Operesheni za kijeshi na mabavu zitaweza tu kuchelewesha sana kufikiwa kwa amani na utulivu
BEIJING – Tarehe 7 Oktoba ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kutimia mwaka mmoja tangu kuanza kwa mgogoro wa sasa huko Gaza, Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning amesema siku ya Jumanne kwamba ukweli wa hali ya uchungu unathibitisha vya kutosha kwamba operesheni za kijeshi na mabavu siyo njia ya suluhu, na itakusanya tu manung'uniko na kusukuma amani na utulivu mbali na kufikiwa.
"Mgogoro wa Gaza umekuwa ukiendelea kwa mwaka mzima, na umesababisha kupoteza maisha ya watu wengi wasio na hatia na kuleta balaa ya ubinadamu ambayo hayajawahi kushuhudiwa," msemaji Mao amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari, akiongeza kuwa kupanuka kwa mgogoro huo kunaathiri eneo zima na kwamba mivutano katika kanda hiyo imeendelea kuongezeka.
“China ina wasiwasi mkubwa kwamba mapigano bado yanaendelea na amani bado ni vigumu kufikiwa,” amesema.
Msemaji Mao ameongeza kuwa si muda mrefu uliopita, China ilipendekeza mpango wa hatua tatu kuhusu mgogoro wa Gaza, ambao unabainisha utatuzi wa dharura ni kusimamisha vita na kutoa msaada wa ubinadamu, "Wapalestina wakitawala Palestina" kama kanuni ya msingi ya ujenzi upya wa baada ya vita huko Gaza na suluhu ya Nchi mbili ni njia ya kimsingi ya kusonga mbele.
“Haki halali za kitaifa za watu wa Palestina zinahitaji kupatikana na wasiwasi wa kiusalama wa Israeli unahitaji kutiliwa maanani,” amesema msemaji Mao.
Jumuiya ya kimataifa inahitaji, kwa msingi wa kuhimiza kupunguza hali ya mgogoro, inapaswa kufanya mkutano wa amani wa kimataifa wenye msingi mpana, maamuzi na heshima, na ufanisi zaidi, na kuandaa ratiba na dira ya utekelezaji wa suluhu ya Nchi mbili, ili hatimaye kufikia kuishi pamoja kwa amani kati ya nchi mbili za Palestina na Israel na vilevile mapatano kati ya Waarabu na Wayahudi, ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma