Lugha Nyingine
Tuzo ya Nobel ya Tiba Mwaka 2024 yawatuza wanasayansi wawili kwa kugundua mircoRNA
Picha za washindi wa Tuzo ya Nobel Mwaka 2024 katika Fiziolojia na Tiba, Victor Ambros na Gary Ruvkun, zikionyeshwa kwenye Taasisi ya Karolinska mjini Stockholm, Sweden, Oktoba 7, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)
STOCKHOLM - Tuzo ya Nobel ya Tiba Mwaka 2024 imetolewa jana Jumatatu kwa wanasayansi wawili wa Marekani, Victor Ambros na Gary Ruvkun, kwa ugunduzi wao wa microRNA na mchango wao katika udhibiti wa jeni baada ya uchanganuzi.
MicroRNAs ni kundi jipya la molekuli ndogo za RNA ambazo ni muhimu katika udhibiti wa jeni. Sasa inajulikana kuwa jenomu ya binadamu ina misimbo ya microRNA zaidi ya 1,000.
Mkutano wa Tuzo ya Nobel umesema kuwa ugunduzi huo wa kustaajabisha wa wanasayansi hao wawili umebainisha mwelekeo mpya kabisa wa udhibiti wa jeni. "MicroRNAs zinathibitisha kuwa muhimu sana katika namna viumbe vinavyokua na kufanya kazi," mkutano huo umeongeza.
Tangazo hilo limeashiria mwanzo wa msimu wa tuzo hiyo ya Nobel mwaka huu. Matangazo ya Tuzo ya Nobel yataendelea kwa kutangazwa washindi wa tuzo ya fizikia leo Jumanne, ikifuatiwa na kemia siku ya Jumatano, na fasihi siku ya Alhamisi.
Tuzo ya Amani ya Nobel itatangazwa siku ya Ijumaa, na Tuzo ya Kumbukumbu ya Nobel katika Sayansi ya Uchumi itatangazwa Oktoba 14.
Tuzo ya Nobel Mwaka 2024 katika Fiziolojia na Tiba ikitangazwa kwenye Taasisi ya Karolinska mjini Stockholm, Sweden, Oktoba 7, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma