Lugha Nyingine
Xi na Kim watumiana salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka 75 ya uhusiano wa kidiplomasia
Rais Xi Jinping wa China na Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) Kim Jong Un, wametumiana salamu za pongezi siku ya Jumapili kwa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na DPRK.
Katika salamu zake, Rais Xi, ameeleza kuwa miaka 75 iliyopita, China na DPRK zilianzisha rasmi uhusiano wa kidiplomasia, na kufungua ukurasa mpya wa historia ya uhusiano wa pande mbili.
Ameongeza kuwa katika miaka 75 iliyopita, nchi hizo mbili zimeungana mikono katika kuimarisha nguvu ya umma na kulinda mamlaka ya kitaifa, kuimarisha mabadilishano na ushirikiano na kuendeleza ujenzi wa ujamaa. Pia zimefanya kazi kwa karibu ili kuhimiza amani na utulivu wa kikanda na kulinda haki na usawa wa kimataifa.
Kwa upande wake, Kim amesema miaka 75 iliyopita, pande hizo mbili zimeshikilia imani zao thabiti katika uhalali wa malengo yao, kushinda majaribu na changamoto mbalimbali, na kusonga mbele kwa ujasiri kwenye njia ya ujamaa.
Kim pia ameelezea imani yake kuwa watu wa China, chini ya uongozi wa CPC na Xi akiwa kiongozi wake mkuu, wataendelea kupata mafanikio mapya katika kujenga nchi ya kisasa ya kijamaa kwa pande zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma