Lugha Nyingine
Mradi wa Awamu ya Pili wa eneo la kuchimba gesi kwenye kina kirefu baharini uliojengwa na China kwa kujitegemea kuanza kufanya kazi (3)
Picha hii ya droni isiyo na tarehe ikionyesha nguzo za jukwaa la uzalishaji wa gesi la Mradi wa Awamu ya Pili wa eneo la kuchimba gesi kwenye kina kirefu baharini uliojengwa na China kwa kujitegemea wa Shenhai Yihao, au Bahari ya Kina Kirefu Na. 1, ulioko umbali wa kilomita 150 kutoka mji wa Sanya katika mkoa wa kisiwa wa Hainan, kusini mwa China. (Shirika la Kitaifa la Kuchimba Mafuta Baharini (CNOOC)/ kupitia Xinhua) |
HAIKOU - Mradi wa eneo la kuchimba gesi kwenye kina kirefu baharini ambao ni wa kwanza kujengwa na China kwa kujitegemea wa Shenhai Yihao, au Bahari ya Kina Kirefu Na. 1, umekamilika ujenzi wa awamu yake ya pili, ambao unatarajia kuanza kazi baadaya muda mfupi siku zijazo, Shirika la Kitaifa la Kuchimba Mafuta Baharini la China (CNOOC), ambalo ni mwendeshaji wa mradi huo limesema Alhamisi.
Kukamilika kwa mradi huo kunaashiria mafanikio makubwa katika uwezo wa China wa ujenzi wa miradi ya kuchimba mafuta na gesi kwenye kina kirefu baharini chini ya hali ngumu, CNOOC limesema.
Mradi huo wa awamu ya pili, wenye akiba iliyothibitishwa ya gesi asilia ya mita za ujazo zaidi bilioni 50, unajumuisha visima 12 vya gesi ya kwenye kina kirefu baharini, jukwaa pana la usindikaji lenye uzito wa tani zaidi ya 14,000 na mabomba matano ya chini baharini yenye urefu wa kilomita takriban 250, kati ya vifaa vingine.
Baada ya mradi huo kuanza kufanya kazi kikamilifu, kilele cha kila mwaka cha pato la gesi asilia la Bahari ya Kina Kirefu Na. 1 kinatarajiwa kuongezeka kutoka mita za ujazo bilioni 3 hadi mita za ujazo bilioni 4.5, CNOOC imeeleza.
Mradi wa Bahari ya Kina Kirefu Na. 1, ulioko umbali wa kilomita 150 kutoka mji wa Sanya katika mkoa wa kisiwa wa Hainan kusini mwa China, unaweza kufanya kazi kwa kina cha zaidi ya mita 1,500 baharini. Ulianza kufanya kazi Juni 2021.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma